Msosi Partner ni nini?
Msosi Partner ni programu tumishi ya simu ya mkononi inayomuwezesha mtumiaji kuuza chakula kutoka katika mgahawa wake na kuwafikia wateja wengi zaidi kwa muda mchache katika jiji la Dar es Salaam.
Msosi Partner hufanya kazi kwa kushirikiana na programu tumishi zingine za Msosidrop na Msosi Dropper. Msosidrop ni kwaajili ya wanunuaji wa chakula ambao ni wateja, na Msosi Dropper ni maalumu kwa ajili wa wasambazaji wa chakula ambao ni madereva wa vyombo vya moto.
Andiko hili ni maalumu kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa wamiliki wa migahawa, wapishi, na mama lishe.
Msosidrop hufanyaje kazi?
Msosidrop hurahisisha mchakato wa usambazaji wa chakula kuwa bora na salama zaidi na kwa wakati kuliko ilivyokuwa zamani.
- Wateja wanaagiza chakula kutoka kwenye mgahawa wako kupitia programu ya Msosidrop.
- Baada ya mteja kulipia, oda hutumwa kwenda kwa mgahawa wako – kwenye programu ya Msosi Partner – kisha utaanza kuitayarisha na kuiwekea alama kuwa ipo tayari kwa kuchukuliwa.
- Madereva wa Msosidrop, maarufu kwa jina la Droppers wataichukua oda hiyo kutoka kwenye mgahawa wako na kuipeleka kwa mteja kwa kutumia Msosi Dropper.
Kwahiyo, mchakato mzima wa usambazaji wa chakula unakuwa rahisi na wa haraka unaomuwezesha mteja kufuatilia muda halisi wa oda yake ilipochukuliwa hadi kumfikia mahali alipo.
Faida za kujiunga na Msosi Partner
Unapohitaji kukuza mauzo mtandaoni, kuvutia wateja, kuongeza oda za wateja, au kuboresha biashara yako, basi Msosidrop tupo kwa ajili yako.
- Vutia wateja wapya – Kwa kuwa mgahawa wako utakuwa kwenye Msosidrop, utaunganishwa na wateja wengi ambao baadhi yao huenda wasiweze kufika mahali ulipo. Hivyo utapanua wigo wa biashara yako.
- Stawi na teknolojia – Utakuza biashara yako na kunufaika kupitia uzoefu wa wataalamu wa Msosidrop, kama vile, uchakataji salama wa malipo mtandaoni, teknolojia ya kufuatilia oda, na kupata takwimu muhimu za mauzo.
- Ongeza mauzo zaidi – Kwasababu mtandao wa Msosidrop unatafuta wateja na wasambazaji, mmiliki wa mgahawa hupati kazi ya ziada. Kazi yako kubwa ni kupika chakula kizuri, safi, na salama.
Zaidi ya hayo, utapata msaidizi wa kiufundi wa Msosidrop ambaye atajitolea kwa ajili ya mafanikio ya biashara yako.
Gharama za Msosi Partner
Hakuna gharama zozote kujiunga na Msosi Partner. Unapaswa tu uwe na intaneti na simu janja.
Baada ya siku 30 za mauzo, utaanza kulipa asilimia 10 kwa kila oda utakayopokea kutoka kwa mtandao wa Msosidrop. Siku 30 huanza kuhesabiwa baada ya kupokea oda ya kwanza.
Kamisheni ya 10% inashughulika na nini?
Ili kuhudumia biashara yako kwa kila kitu tunachofanya, tunachukua kamisheni ya asilimia 10 tu kwa oda zinazochakatwa nasi. Hapa kuna baadhi ya gharama ambazo kamisheni hii hufanya:
- Utangazaji na uuzaji – Tunangaza na kuuza biashara yako kwa wateja wapya kila siku.
- Gharama za kusafirisha – Tunawawezesha madereva kujiajiri, kwa kuwapa fursa rahisi za mapato kupitia kusambaza chakula.
- Huduma kwa wateja, migahawa, na madereva – Kwakuwa wateja, wamiliki wa migahawa, na madereva wana mahitaji ya kipekee ambayo mara nyingi yanahitaji majibu ya haraka. Tuna timu ya huduma kwa wateja iliyo tayari saa 24 kila siku kusaidia kutatua matatizo ya wateja wetu.
- Gharama za uendeshaji wa programu – Tumeajiri vijana walio bora, wenye ujuzi, wahandisi wa mifumo ya komputa, na wajuao kutumia teknolojia mpya kuhakikisha programu tumishi zote tatu zikifanya kazi bila kusimama. Tarajia huduma bora kutoka kwetu.
- Gharama ya mchakato wa malipo – Kwa kuunganishwa na Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money na akaunti yako ya benki, huna wasiwasi mwingi kuhusu gharama za malipo ya ziada.
Jinsi ya kujiunga na Msosi Partner
Kujiunga na Msosi partner ni rahisi sana. Hapa kuna hatua ambazo utahitaji kuzifuata:
- Nenda kwa ukurasa wa usajili wa merchant
- Jaza jina na anwani ya mgahawa wako.
- Jaza baadhi ya taarifa za msingi za mawasiliano (jina lako, nambari yako ya simu, anwani ya barua pepe).
- Kagua maelezo yako na utume ombi lako.
Baada ya kutuma ombi lako, timu ya Msosidrop itawasilina nawe ili kukamilisha usajili wako.
Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu namba +255 658 634 619.